Masanja Mkandamizaji Amvalisha Pete ya Uchumba Monica
Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi Masanja Mkandamizaji Jumapili hii amemvalisha pete mpenzi wake aitwae Monica akijiandaa safari ya kufunga pingu ya maisha.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mchungaji, Jumapili hii akiongezana na ndugu zake wa karibu pamoja na wasanii wenzake katika kanisa la Mito ya Baraka, aliweza kumvalisha pete mchumba wake Monica.