Picha: TRA Wanaipiga Mnada Range Rover Evoque ya Wema Sepetu
Gari aina ya Range Rover Evoque 504 ambayo Wema Sepetu alijizawadia kwenye birthday yake mwaka jana inapigwa mamlaka ya mapato tanzania (TRA) baada ya hivi karibuni mamlaka hiyo wanaishikilia gari hiyo kwasababu iliingizwa nchini bila kulipiwa kodi na kwakuwa ushuru wake ni takriban nusu ya gharama yake, Wema ameshindwa kuikomboa.
Ipo mnadani kwa bai ya takriban shilingi milioni 200.
Kuna tetesi ziliwahi kuandikwa kuwa gari hilo hata hivyo alipewa kama zawadi na pedeshee wa Kongo anayedaiwa pia kuwahi kuwa na uhusiano na Jacqueline Wolper.