Stan Bakora: Vijana Tusipende Mteremko
MKALI wa vichekesho nchini, Stanley Yusuph ‘Stan Bakora’, anatarajia kuachia filamu yake ya kwanza itakayoitwa ‘Shobodundo’ iliyobeba mafunzo kwa vijana wanaopenda maisha mazuri bila kujishughulisha.
Stan Bakora alisema kutokana na hilo vijana wengi wamejikuta wakilazimika kulelewa na wanawake watu wazima wenye uwezo mkubwa kifedha bila kujali kwamba wao ni nguvu kazi ya taifa.
“Kiukweli hii filamu itawakera vijana wengi wanaopenda maisha ya mteremko ‘marioo’ na itawafurahisha wanaopenda kuwajibika kupitia shughuli mbalimbali za kuajiriwa na binafsi,” alieleza Stan Bakora.
Filamu hiyo inatarajiwa kusambazwa mwishoni mwa mwezi huu huku ikiwa imeshirikisha wasanii mbalimbali nyota akiwemo Batuli, Kitale na Pinky.
Mtanzania