Watoto wa Mastaa wa Bongo Wanaotabiriwa Kuja Kuwa Mastaa
Kila mtoto anapozaliwa huanza kumuangalia mzazi wake kama ni role model wake, lakini baadaye wengi huanza kubadili mawazo yao.
Mastaa wa Bongo wameanza kuwatengenezea mazingira watoto wao ya kutembelea nyota za wazazi wao ili watengeneze hela kuanzia sasa mpaka hapo baadaye.
Hawa ni baadhi ya watoto wa mastaa wanaotabiriwa kuja kuwa mastaa baadaye, wengine wanaweza wakawa na majina makubwa kuliko ya wazazi wao.
Latifa Nasibu (Tiffah)
Mpaka sasa ana umri wa miezi saba na siku kadhaa, Tiffah amekuwa ni staa pia ana followers kibao kwenye akaunti yake ya Instagram. Kutokana na umaarufu aliokuwa nao baba yake, Diamond na mama yake Zari, Tiffah ameshapata dili kadhaa ambazo zinamuingizia pesa kwa sasa huku akiwa bado hajui nini kinachoendelea.
Tiffah ni balozi wa Msasani Mall & Pugu Mall, pia ni balozi wa NMB Junior Account hii ni akili pekee iliyotumiwa na Diamond Platnumz na Zari ambayo inaweza ikamfanya Tiffah akatumia fursa hiyo kuja kuingiza hela nyingi hapo baadaye na akawa maarufu zaidi duniani.
Kendrick Mabeste
Mabeste na Lisa wanajivunia kuwa na mtoto kama Kendrick, akiwa anakaribia umri wa miaka mitatu, Kendrick ameshaanza kuwa maarufu na kuingiza mkwanja wake binafsi kwa kufanya baadhi ya matangazo.
Pia Kendrick amewahi kuwa mshindi kwenye shindano la Tabasamu akiwa ni mtoto mwenye kupendeza kwenye picha (Photogenic). Nje ya kufanya matangazo watu wameanza kumtabiria Kendrick kuja kuwa rapper kama baba yake (Mabeste).
Tanzanite Hamisi
Madini ya Tanzanite yana patikana Tanzania pekee, japo nchi ya India ndiyo inaonekana ni ya kwanza kwenye kuuza madini hayo. H Baba na Flora Mvungi hawakukosea kumuita mtoto wa jina la Tanzanite, ni mmoja kati ya watoto wa mastaa wenye mvuto na wenye muonekano mzuri.
Tanzanite yupo chini ya menejimenti ya Lisa Karl Fickenscher, ambaye anamsimamia Kendrick pia. Koffie Olomide aliwahi kumweka Tanzanite kwenye Instagram yake baada ya kushinda shindano ambalo Koffie alilitoa mtu ajirekodi akiimba wimbo wa Ekotite na kuahidi atakaye shinda angewekwa kwenye Instagram yake.
Pia alipata mualiko wa kushiriki mashindano ya U miss kwa watoto ambayo yalifanyika nchini Rwanda. H. Baba aliwahi kusema “kuwa kuna matangazo mengi ambayo Tanzanite anatakiwa kuyafanya kwa sasa.”