Maisha ni Kupambana- Alex Sanchez
Kama ulikuwa hufahamu, haya ni machache kuhusu mchezaji Alex Sanchez ambaye teyari ameshajiunga na Manchester United.
Alimuepusha mama yake na kifungo.
Baba yake Sanchez aliachana na mama yake kabla ya yeye Sanchez kuzaliwa. Baada ya kuzaliwa na Ili kumlea mtoto wake mama yake aliaanza biashara ya kuuza samaki. Na akiwa na umri wa miaka 16 mama yake alishtakiwa kwa kosa la kuuza samaki bila leseni na kupigwa faini ya dola 1,000. Mama yake hakuwa na hizo fedha na ilibidi mipango ifanyike kwa wakala wa mchezo wa kabumbu kwa makubaliano kuwa hilo deni litalipwa lakini Sanchez atakuwa chini ya wakala huyu kwa muda wote wa uchezaji wake.
Mtu wa kukwea miti na mapaa ya nyumba.Jina lake la utani akiwa kijana mdogo alikuwa anaitwa ‘Dilla’ kwa lugha ya Kihispania akifananishwa na mnyama mdogo aina ya Kindi (Squirrel). Jina hili la Dilla alilipewa kwa sababu ya umahiri wake wa kukwea miti na mapaa ya nyumba.Ilimchukua sekunde kukwea au kupanda mti au kufikia juu kwenye mapaa ya nyumba nyingi za mtaani kwao ambapo alipanda kwenda kuchukua mipira iliyokuwa imenasa. Ole wako akukimbize halafu ujifanye unapanda mtini ili asikukamate, itakula kwako!
Ni Mkimbiaji Mashuhuri. Akiwa anachezea timu ya Udinese ya nchini Italy, siku moja alienda mjini na gari yake na kwa bahati mbaya akapoteza ufunguo wa gari yake. Badala ya kuomba lift ili arudi nyumbani kuchukua ufunguo wa pili, aliamua kutoka nduki kwenda hadi nyumbani kuchukua ufunguo mwingine. Alikimbilia kilometa karibu 7 kuufuata ufunguo wa akiba. Hapa walinzi wa timu pinzani wanahaha sana maana anakimbia kupita maelezo.
Guardiola amenifanya nijisikie kama a Ferrari.’ Licha ya kwenda kuchezea mpira ktk timu ya Manchester United kwa dau kubwa duniani bado anasema hatamsahau kocha wa Manchester City kwa mchango wake mkubwa ktk soka lake hadi kuweza kujisikia mwenye hadhi ya kifahari kama magari ya bei ghali Duniani ya Ferrari.
Hakuwa na viatu vya kuchezea mpira- Alikuwa akiazimiwa na mama yake.Kiatu chake cha kwanza cha kuchezea mpira aliweza kukipata kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 15. Kabla ya hapo mama yake alikuwa anamuazimia na baada ya mechi anarudisha.
Mchezaji mwenye umri mdogo kwenye timu ya taifa : Aliweza kuchezea timu ya taifa ya Chile akiwa na umri mdogo kuliko wote na hadi leo ndiye mpachikaji mabao mengi kuliko wote walio wahi kuchezea timu ya taifa akiwa ameshafunga mabao 39.
Ataingia Kuigiza sinema :Sanchez amesema baada ya kustaafu kucheza mpira atapendelea kuwa mcheza sinema.
Alexis Sanchez – Welcome to Manchester United – Crazy Skills Show, Passes & Goals – 2018.