-->

Wema Atimuliwa Kwenye Nyumba

UFALME umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni 280, fuatana na Ijumaa Wikienda.

WEMA SEPETU66
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18, mwaka huu.
SIKIA CHANZO
“Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.”

wema761
BABA MWENYE NYUMBA AINGIA KATI
“Sasa baba mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini akamtaka Wema ahame haraka kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.
SIKU YA TUKIO
Paparazi wetu alizidi kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa, muda huo tayari kuna lori aina ya Toyota Canter linahamisha vitu nyumbani kwa Wema na kwamba, kuna kila dalili anahama baada ya baba mwenye nyumba wake kumtimua.
PAPARAZI NYUMBANI KWA WEMA
Ilibidi paparazi wetu akimbie kwa pikipiki iendayo kasi mpaka nyumbani hapo na kukuta kweli lori likibeba vitu mbalimbali huku wabebaji wakitokwa jasho chapachapa.
Gari hilo lilisimama kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba hiyo huku likiwa na shehena ya mafurushi ya mizigo.
Wakati paparazi wetu akiwa kwenye hali ya mshangao, aliendelea kuona mizigo mbalimbali ikitoka ndani ya mjengo huo huku vyombo anuai vya ndani, kama kabati na baadhi ya makochi yakiwa nje ya nyumba hiyo yakisubiri kupakiwa tayari kwa safari ya kumuondoa Wema kwenye mjengo huo.
WEMA HAYUPO
Swali la kwanza kwa wabebaji hao kutoka kwa paparazi wetu ni wapi alipo Wema.
“Unamtaka Wema wa nini wakati unajua hayupo hapa, kwanza wewe nani?” alikuja juu mpakiaji mmoja.
PAPARAZI ANUSURIKA KIPIGO
Katika hatua nyingine isiyokuwa ya kawaida, wapakiaji wengine walitaka kumshushia kipigo paparazi wetu baada ya kuona mwanga wa kamera wakati akichukua picha kadhaa kwa ajili ya ushahidi.
WALIKOHAMIA
Uchunguzi wa awali, Wema amehamia Mbezi Beach, Dar. Hata hivyo, tangu sakata la wizi wa maji na umeme, Wema hajawahi kulala na kuamka ndani ya nyumba hiyo huku habari zikisema amekuwa akiishi mahotelini kama ‘digidigi’.
KWA NINI WEMA ALISEMA NYUMBA NI YAKE?
“Kuna watu wengi walikuwa hawatambui kwa nini Wema awali alisema hii nyumba ni yake. Mwanzo wakati anahamia, pia alikuwa ana mazungumzo na baba mwenye nyumba kwamba ainunue lakini watoto wakagoma hivyo Wema akawa analipa kodi kila mwaka.
WEMA, PETIT MAN
Juzi, Wema hakupatikana hewani ili kujibu madai hayo, lakini mmoja wa watu wake wa karibu, Petit Man alikumbana na paparazi wetu katika klabu moja jijini Dar, alipoulizwa kuhusu mambo hayo alikiri Wema kuhama kwenye nyumba hiyo.
“Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach,” alisema Petit.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364