-->

Shamsa Ford: Sitaki Tena Kutoka Kimapenzi na Mastaa

Msanii wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford amesema amekoma kutoka kimapenzi na watu maarufu.

Shamsa Ford

Shamsa Ford

 

Muigizaji huyo ambaye miezi michache iliyopita alikiri kutoka kimapenzi na rapa Nay wa Mitego, ameiambia Bongo5 kuwa sasa hivi amepata mpenzi mpya ambaye atamweka wazi siku ya harusi yake.

“Mimi ni mwanamke mzuri nakosaje mwanaume? Nimetimia kila idara, nina mchumba ambaye tunapendana Mungu akijalia kiukweli natamani awe mume wangu,” amesema.
“Nimeshatangaza kabisa mastaa sitaki nimekoma, nimekoma kutoka kimapenzi na mastaa au kumtangaza mpenzi wangu kwenye mitandao. Mpenzi wangu watamjua siku ya harusi yangu. Unajua mastaa wana mambo mengi sana na kuendelea nao ni kupoteza muda tu” amesisitiza Shamsa Ford.

Hata hivyo Shamsa hakutaka kuzungumzia sababu ya kuachana na Nay.

Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364