-->

Sitoki na Mwigizaji Yoyote Bongo Movie- Rachel

MSANII wa filamu Bongo Rachel Bitulo amefunguka kwa kusema kuwa hana mahusiano na mwigizaji yoyote kwani yeye ana mchumba wake ambaye wanapenda sana hivyo hawezi kuwa uhusiano na msanii wa filamu awe mkubwa au mdogo hata usumbufu uvumi huo unakuja baada picha moja kurushwa mtandaoni.

Rachel Bitulo

Picha hiyo alikuwa na mwigizaji mwezake Stanley Msungu maarufu kama Senator wakiwa katika hali ya mahaba na kuzusha maswali mengi kwa watu na wengine moja kwa moja wakadai kuwa wasanii hawa ni wapenzi na wana mahusiano kwa muda mrefu kutokana na ukaribu wao.

“Msungu mimi ni kaka yangu na namheshimu picha ile ilikuwa location wale si chumbani au sehemu nyingine ambapo unaweza kufanya mambo ya ajabu, namwachia mungu kwa aliyefanya hivyo,”alisema Rachel kwa huzuni.

Rachel akiwa na Msungu akimkamua chunusi kimahaba

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364