-->

Mimi ni Chawa kwa Matajiri – Shetta

Msanii Shetta ametaka watu wasimuhisi kuwa anajishughulisha na biashara za madawa na badala yake watambue yeye ni mtu anayetumia fursa kila aonapo na ndio maana ana marafiki wengi matajiri ambao wanamsaidia.

Msanii Shetta

Akizungumza kwenye Planet Bongo East Africa radio, Shetta amesema kwamba yeye hajishughulishi na biashara hizo za madawa na wala hana pesa za kutisha kama jinsi watu wanavyomfikiria.

“Mimi sina fedha nyingi kama watu wanavyodhani, sema nina fedha za kutosheleza maisha yangu. Ningekuwa nina pesa nisingwekuwa nawaganda matajiri. Mimi ni chawa kwa matajiri nikiwa nashida namcheki boss Mo, au matajiri ambao nimetengeneza ukaribu nao na mwisho wa siku mambo yangu yanaenda,” Shetta.

Katika hatua nyingine Sheta amesema yeye ni mtu ambaye anapenda vitu vizuri na ndiyo sababu watu wengi wamekuwa wakimfikiria vibaya

‘Ningekuwa nauza madawa ningekuwa na mimi kwenye ile orodha iliyowahi kupelekwa pale polisi. Mimi ni mtu ambaye napenda vitu vizuri na nikikitaka nitakipata. Kwa hali ya kawaida ukiangalia kazi tunazozifanya huwa zinatulipa, kwa hiyo mimi kuwa na vitu nilivyonavyo vinaendana na kipato ninachokifanya. Yapo matangazo mengi na nimekuwa balozi wa makampuni mbalimbali na yote hayo yananilipa na siyo siri maana watu wanatambua” – aliongeza.

Kwa sasa Shetta anatamba na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Wale wale’ baada ya kukaa muda mrefu kimya

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364