-->

Lulu Diva: ‘Milele’ Ilinipa Wakati Mgumu

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Lulu Abasi ‘Lulu Diva’, amesema wimbo wake unaoitwa ‘Milele’, ndio uliompa wakati mgumu tangu alipoanza kujihusisha na tasnia ya uimbaji.

Lulu Abasi ‘Lulu Diva’

Akizungumza hivi karibuni na MTANZANIA, Lulu Diva, alisema ugumu ulianza wakati wa kuandaa wimbo huo, hadi kukamilisha.

Alisema licha ya kuwa wimbo huo ulimtambulisha vema katika tasnia ya muziki hapa nchini, lakini ulimpa changamoto kubwa ambazo zimebaki kama kumbukumbu kwenye maisha yake.

“Wimbo wangu wa Milele ninauheshimu sana, umenitoa na kunitambulisha katika ulimwengu wa muziki, ila ulinipa wakati mgumu sana kuhakikisha unakamilika,” alisema Lulu Diva.

Lulu Diva alisema wimbo huo ambao video yake ilifanyika nchini Afrika Kusini chini ya mtayarishaji Nicholaus, ulimpa nafasi ya kufika nje ya nchi kwa mara ya kwanza.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364