Barack Obama Asema Haya kwa Wakenya
Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, amewataka wananchi wa Kenya kufanya uchaguzi mkuu kwa amani bila vurugu .
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, Bw. Obama ametoa wito pia kwa viongozi wa Kenya kukataa vurugu na uchochezi na kuheshimu maamuzi ya wananchi.
Kiongozi huyo wa zamani,ambaye baba yake mzazi ni mzaliwa wa Kenya amewasisitizia Wakenya wote kuufanyia kazi uchaguzi huo ili kuhakikisha ni wa amani, unaoaminika hali ikatakayoongeza imani kwa Katiba Mpya ya nchi hiyo na mustakabali wa taifa hilo.
Uchaguzi wa leo unaelezwa kuwa ni mtihani kwa Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 uliogubikwa na vurugu zilizodumu kwa miezi miwili na kusababisha watu 1,100 kupoteza maisha na wengine laki sita kuyakimbia makazi yao.
EATV.TV