Msami: Haikuwa Rahisi Kumbadili Chemical
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Msami Giovani ameeleza jinsi alivyopata wakati mgumu kumbadilisha kimavazi Claudia Lubao ‘Chemical’ aliyezoeleka kwa mavazi yake ya kiume ili avae kikekike katika video ya wimbo wake wa So Fine.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Msami alisema aliona mtu anayefaa kufanya naye hiyo ngoma yake ni Chemical hivyo akambadili kimavazi ambapo kwenye video ya wimbo huo alionekana akiwa amevaa gauni, wigi pamoja na kupaka make-up, jambo ambalo halikuwa rahisi.
“Ni kweli watu wengi wamestaajabu kumuona Chemical akiwa amevaa gauni, nilivyoenda na wazo la kufanya naye ile ngoma nilimwambia lazima aonekane kwenye video pia, ambapo mwanzo kulikuwa na ugumu maana kumbadilisha mtu kwenye swaga alizozizoea si kitu kidogo, mwisho wa yote akalegeza kamba akakubali,” alisema Msami.
Chanzo:GPL