Mh. Ester Bulaya Kuletwa Muhimbili na Ndege
Hali ya Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mh. Ester Amos Bulaya imezidi kuwa mbaya, kwa mujibu wa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Mh. Joyce Sokombi, ambaye yuko naye hospitali akimuuguza.
Mh. Sokombi amesema pamoja na kwamba amepelekwa katika hospitali ya mkoa Mara Mbunge huyo hajapata nafuu, hivyo amepewa rufaa ya kuja hospitali kuu ya Taifa Muhimbili.
Ester Bulaya alipata matatizo ya presha na kukimbizwa hospitali hapo jana huku akiwa kizuizini, na kwa sasa yuko nje kwa dhamana.