-->

Wema Sepetu Asaka Mtu Wakutoka Naye

Msanii wa filamu wa kike bongo Wema Sepetu ambaye wengi humtaja kuwa msanii mwenye nyota ya kupendwa na mashabiki, amefunguka kuwa anasaka mtu atakaye toka naye usiku wa uzinduzi wa filamu yake.

 

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amendika ujumbe wa kumtafuta mtu huyo atakayekuwa naye usiku huo, kwani akisema raha ya tukio kama hilo lazima uwe na mtu pembeni yako, kwani anatarajia kuvunja kabati kwa kupendeza, lakini haitakuwa na maana kama atakuwa peke yake.

” Bado siku 4 tu, nilisema kuna tatizo, kupendeza nitapendeza tena sana tu ila sasa sina date wa kwenda naye raha ya zulia jekundu uwe na mtu… nani atajitolea kuwa mtu wangu kwa usiku huo wa kukumbukwa!?”, aliandika Wema Sepetu.

Mwisho wa wiki hii Wema Sepetu anatarajia kuzindua filamu yake mpya inayoitwa ‘Road to heaven’ aliyoigiza na wasanii wengine wakali wa filamu, akiwemo mshindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kiume EATVAwards 2016, Gabo Zigamba, muigizaji wa kike Grace Mapunda na Petit Man.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364