-->

Jux Aendelea Kumng’ang’ania V Money

LICHA ya ‘couple’ ya mastaa Vanessa Mdee ‘V Money’ na Juma Mussa ‘Juma Jux’ kufikia mwisho, Jux ameibuka na kusisitiza kuwa, atendelea kuwa karibu na mwanadada huyo kwa kuwa bado anampenda.

Jux na V money enzi za penzi lao

Jux alisema ni kweli wameachana, baada ya kushindwa kufikia mwafaka wa tatizo lao, lakini wataendelea kuwa karibu kutokana na ustaa wao na urafiki.

Akizungumza na MTANZANIA, Jux alisema wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa miaka minne, lakini kila mmoja ameridhia uhusiano wao kufikia ukingoni na sasa wataendelea kuwa karibu katika kazi zao.

“Nimekuwa katika mahusiano na Vanessa kwa miaka minne, kabla ya hapo tulikuwa marafiki wa muda mrefu, tumeshindwa kufikia mwafaka na ndiyo maana kila mmoja ameridhika kuachana kwetu, ingawa watu watambue kuwa wataendelea kutuona pamoja kwa sababu sisi ni watu maarufu na tutaendelea kufanya kazi pamoja,” alisema Jux.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364