BASATA Yakanusha Kuifungia “Zari All White Party”
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekanusha taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa limelifungia onesho la mpenzi wake Diamond, Zari, ‘Zari White Party’.
Moja kati ya mitandao iliyoandika story hiyo ni Jamii Forums, ambapo walidai BASATA imelifungua onesho hilo kufanyika hapa nchini.
Kupitia ukurasa wa Twitter, BASATA limekanusha taarifa hizo huku likiwataka wananchi kupuuza taarifa hizo.
1/2:Kuna uvumi unaenezwa kwenye mitandao ya kijamii & baadhi ya vyombo vya habari kutupigia simu kwamba kinachoitwa White Party kimefungiwa
— Baraza la Sanaa (@BasataTanzania) January 21, 2016
2/2:Tunapenda kueleza kuwa habari hizo si za kweli ni za uzushi.Zipuuzwe.Pengine zinaratibiwa na watu wenye malengo yao. Wapuuzwe.
— Baraza la Sanaa (@BasataTanzania) January 21, 2016
Bongo5