-->

VIDEO: Wema Afungukia Ishu Yake na Mbowe

Malkia wa filamu bongo, Wema Sepetu amekanusha kuwa na mahusiano na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe ambaye miezi michache iliyopita alihusishwa kutoka naye baada ya sauti zinazodhaniwa kuwa za kwao  kusambaa mitandaoni.

Wema amesema kuwa katu hajawahi kuwa na mahusiano na kiongozi huyo wa upinzani kwani ni mtu ambaye anamuheshimu sana na kuongeza kwamba sauti hizo zenye mazungumzo ya faragha zilitengenezwa na watu asiowafahamu wenye nia ya kumchafua.

Akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Nirvana, Deogratius Kithama, Wema Sepetu amesema anashindwa kuelewa sauti  hizo zilipotokea kwani anamuheshimu sana Mh. Mbowe na heshima yake hiyo wakati mwingine inampa hali ya kumuogopa hivyo anaamini kitendo hicho kilitengenezwa na watu wenye nia ya kuwachafua kisiasa.

“I was shocked, sijui chochote kuhusu hicho kitu. Mimi mwenyewe sijui kilipoanzia na kwanza ninavyomuheshimu yule baba mpaka namuogopa sasa hili lilipotokea i was like hizi ni figisu. Ingawa sijakutana na Mbowe toka jambo hili kutokea kwa sababu yupo busy lakini viongozi wengine wa CHADEMA walinielewesha ni kwa nini watu wanafanya hivyo. Wema Sepetu

Wema ameongeza ” Unajua hizi ni siasa. Huku ni upinzani na wengine ndiyo wapo madarakani so mambo kama haya ya kisiasa yanatokea ingawa huyo aliyetengeneza sauti kufanana na ya kwaangu yupo vizuri sana.

Sauti ya Wema pamoja na Mbowe ilivujishwa miezi michache baada ya muigizaji huyo pamoja na mama yake kuhamia upinzani wakitokea CCM kwa madai ya kutaka kutumikia chama chenye demokrasia ya kweli

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364