Wolper Afunguka Kumtolea Mahari Mchumba Wake
Msanii wa filamu bongo mwenye mvuto wa kipekee Jacline Wolper, amefunguka kuhusu suala la kumtolea mahari mchumba wake ambaye yuko naye kwa sasa, na kusema kwamba si kweli kama anataka kumtolea mahari huku akigusia harusi yao.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Wolper amesema habari hizo hazina ukweli wowote kwani sio suala la mahari tu, hata mipango ya ndoa baina yao haipo kabisa.
Jackline Wolper aliendelea kusema kwamba kiutaratibu wanaume ndio wanaozungumzia suala la ndoa na sio wanawake, na kwamba hawezi kuvunja miiko ya asili yake kwani wazazi wake hawatafurahia.
“Hamna harusi wala hamna mahari, masuala la ya harusi wanaongeaga wanaume, nikitoa mahari ntakuwa nimeshakuwa muhindi, maana wahindi ndio wanawake wanatoa mahari, sasa mtoto wa kichaga useme unatoa mahari baba yako si atakukana! wanavyopenda ng’ombe na mbuzi”, alisema Wolper
Wolper kwa sasa yupo kwenye mahusiano na kijana anayefahamika jina la Brown, baada ya kuachana na msanii aliyekuwa naye kwenye mahusiano, ambaye alishampeleka mpaka nyumbani kwao.
eatv.tv