-->

Wema Sepetu na Idris Kazi Bado Ipo

INSTAGRAM siku hizi ndo imekuwa sehemu ya watu wengi maarufu kutolea mapovu yao mengi pengine inaweza ikawa sababu ya umaarufu wa mtandao huo na uwepo wa watu wengi wanaotumia pia.

Majuzi kolabo hatari ambalo liliingia doa mapema, kati ya Idris Sultan na Wema Sepetu lilianza kuonekana tena kuanza kurudi rudi baada ya wote kwa pamoja kutokea wakiwa pamoja katika usiku wa uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu wiki chache zilizopita.

Lakini si muda hali ilichafuka baada ya Idris kuzindua viatu vyake ambapo Wema yeye hakutokea ambapo mwanadada Wema aliweza kutoa povu zito katika Instagram yake akiomba msamaha kwa kitendo hicho.

Wema katika posti hiyo anasema jambo kubwa lililosababisha kukosekana katika sherehe hiyo ni kutokana na nguo aliyotakiwa kuvaa kuharibiwa hivyo kushindwa afanye nini.

Wema anadai Idris hapokei simu yake hivyo kaamua kuomba msamaha kwa njia hiyo ambayo anaona ingeweza kumfikia vizuri na kweli iliwezekana sababu ni kama mashabiki wa Wema walihamia kwenye ukurasa wa Idris wakimuombea msamaha kipenzi chao.

Idris katika mahojiano na mwandishi, anasema yeye hana noma na ashapotezea jambo hilo.

“Sina noma yoyote, nishapotezea sababu ni mshikaji, kitu cha kawaida tu,”

Alipoulizwa juu ya suala la kumpenda bado Wema, Idris alikataa kujibu swali hilo na kisha kupotea hewani.

“Hilo swali naomba nilitunze tu kwanza,” alimaliza.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364