-->

Wolper Afunguka Kama Akitendwa na Mpenzi Wake Wasasa

Muigizaji wa filamu na Mfanyabiashara, Jacquline Wolper amefunguka na kusema iwapo mpenzi wake wa sasa (Brown) akimtenda na kumuumiza kama waliopita ataamini kuwa hakuna wa kumwamini kwenye mapenzi na kwamba wanaume wote wana matendo ya kufanana.

Akizungumza na Mwandishi wa EATV, Wolper ambaye miezi michache alitangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake (Msanii wa muziki) ma kisha kuweka wazi mahusiano yake na Mwanamitindo Brown amesema kutokana na kijana huyo pamoja na familia yake kuwa na imani ya dini anaamini hataweza kumuumiza ingawa binadamu wana mapungufu.

“Siamini kama BFF anaweza kunifanyia vitendo vibaya kama nilivyowahi kufanyiwa. Namuamini sana kutokana na kuwa na hofu ya Mungu lakini bado sisi ni binadamu. Anaweza kunikosea kawaida au mimi nikamkosea kwa sababu sisi ni binadamu hiyo haitafanya nimchyukie lakini akifika huku pa kunifanya niumie kama nilikotoka nitaamini kuwa hakuna wa kumuamini,” Wolper.

Wolper amesema kuwa, Brown ni aina ya mwanaume ambaye alikuwa akimuhitaji katika maisha yake na hatimaye Mungu kasikia kilio chake

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364