-->

AliKiba Amefungukia Picha Zilizozagaa Mitandao

Dar es Salaam. BAADA ya picha kadhaa kutembea katika mitandao ya kijamii ikimuonesha AliKiba akiwa na mrembo mmoja picha ikionesha wakiwa kitandani.

Watu walianza kudai kuwa mrembo huyo atakuwa mpenzi wake mpya lakini AliKiba amekanusha suala hilo na kusihi mitandao ya kijamii watu kuitumia vizuri.

Baadhi ya vyanzo vinasema kuwa mrembo huyo ni Dada yake na H-Baba ambae ni shabiki mkubwa wa AliKiba na picha ilipigwa wakati AliKiba akiwa Mwanza na picha kusema kuwa ilipigwa eneo la mapokezi ambapo wasanii wengi walifikia kwaajili ya tamasha la Fiesta.

“Ni ujinga tu, kwanza pale watu wanaona ni kama kwenye mapokezi,sema kwa sababu watu wameamua kuongea acha waongee lakini katika hilo wanalofikiria hakuna ukweli wowote,” alisema AliKiba.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364