Ben Pol: Sijafikiria Kuoa kwa Sasa
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Pol, amefunguka na kusema bado hajafikiria kuoa kwa sasa, kwani bado anahitaji kupambana na maisha ili kutimiza malengo aliyojiwekea.
Akizungumza jana, Ben Pol alisema kupata mke mwema ni kazi, hivyo bado ana safari ndefu ya kuhakikisha anatengeneza maisha kwanza halafu ndoa ifuate.
“Sijapanga kuoa kwa hivi karibuni, kiukweli bado nina safari ya kupambana na maisha ili nifanikishe malengo yangu ya kimaisha ambayo nimejiwekea,” alisema Ben Pol.
Alisema kuwa, mwanamke anayemhitaji si lazima awe maarufu, bali ni yule mwenye mawazo ya kimaendeleo ya maisha ambaye hofu ya Mungu inaishi ndani yake.