-->

Wema Sepetu Ainunua Instagram kwa Muda

Mrembo Wema Sepetu siku ya jana ni kama alinunua mtandao wa Instagram kwa muda baada ya picha zake kutawala.

Katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa, wasanii mbalimbali na watu wengine mashuhuri walipost picha ya mrembo huyo kumtakia kheri ya kuzaliwa hivyo kufanya mtandao mzima kutapakaa kwa picha zake.

Moja ya watu maarufu waliomtakia kheri ya kuzaliwa ni Diamond Platnumz, Jokate Mwegelo, Idris Sultan, Hamisa Mobetto, Van Vicker na wengine wengi tu.

Lakini watu wengi walikuwa na hamu ya kuona namna ambavyo watu kama Diamond Platnumz watavyo mpost pamoja na Idris Sultan ambapo kwa upande wa Diamond aliweka picha ya Wema akiwa na Idris na kumtakia kheri jambo lililozua maswali mengi kwamba jamaa anawapatanisha au anataka kuwakoleza warudiane tena.

 Idris aliandika “Kuna mtu kapewa ruksa ya kusema chochote anachokitaka leo sasa nimekua mtumwa naomba tu siku iishe na chochote nitakachofanya leo jueni sio mimi jamani nimetekwa na wasiojulikana. Pichani juu ni mdada akiangalia kitu ambacho ningemuomba aniachie nipambane nacho leo hicho ndio kitengo. Hii ni picha ya 4443, ya 4444 itakua kesho na itakua habari nzitoooooo sanaaaaaaaaaaaaa  ila kwa sasa acha nirudi utumwani siku iishe” alimaliza.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364