Mapenzi Kwangu Yanashika Nafasi ya Nne-Vanessa
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee ‘V-Money’, ameeleza vitu vinne vilivyopewa nafasi kubwa katika maisha yake, huku mapenzi yakishika nafasi ya mwisho.
Akizungumza hivi karibuni na MTANZANIA, mwanadada huyo alisema ameamua kuyapa mapenzi nafasi ya mwisho ya nne ili kuongeza juhudi katika vitu vya maana.
V-Money alisema kitu kilichopewa nafasi kubwa na kinachoshika namba moja ni Mungu, huku jambo la pili likiwa ni familia na tatu ikiwa ni muziki.
“Muziki nauchukulia kama kazi, sababu ndiyo kitu kinachoweza kuniingizia kipato changu cha kila siku,” alisema V-Money.
Alisema ikiwa ataingia tena kwenye mahusiano mengine ya kimapenzi, anapenda kupata mtu mwenye upendo wa dhati na kuthamini kila kinachofanywa kwa ajili ya maendeleo.
Mtanzania