-->

Kajala Masanje Aoneshwa Akimtega Shemeji Yake

Video mpya ya ‘Omulilo’ ambayo ni kazi yake mwanamama Saida Karoli imeachiwa rasmi, huku Kajala akiigiza muhusika aliyeimbwa kwenye wimbo huo.

Video hiyo inamuonyesha Kajala akiwa anaishi kwa shoga yake kipenzi, lakini licha ya kumsitiri anafanya kitendo kibaya cha kumtaka shemeji yake kimapenzi kwa kumtega kwa kumvalia mavazi ya kumshawishi.

Kazi hiyo ambayo imefanywa na mikono ya Hanscana, ni moja ya kazi zilizoachiwa hivi karibuni na Saida karoli tangu arudi rasmi kwenye game, baada ya kishindo cha wimbo wa ‘Orugambo’.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364