Pastor Myamba Anatoa Mapepo Kanisani Kwake Kigamboni
HISTORIA ya tasnia ya filamu imekuwa ikiendana na uhalisia wa waigizaji katika kujenga uhusika na kuwa ndio maisha halisi, ukiona muigizaji anaigiza mtu wa kaleti itakuwa hivyo, hilo linajitokeza kwa Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ ambaye naye kwa sasa pamoja na kumiliki chuo cha Sanaa sasa anamiliki kanisa lake Kigamboni.
“Naamini kuigiza ni sehemu pia ya kuhubiria maana filamu ni njia ya kufikisha ujumbe kwa hadhira, hivyo ninaigiza lakini pia ni natoa huduma ya kiroho katika kanisa la The World of life Ministry kama mchungaji,”alisema Pastor Myamba.
Pastor Myamba ni moja kati ya wasanii waliobobea katika kuigiza nafasi za filamu za Kidini akiigiza kama mchungaji na alijipatia umaarufu sana alipoweza kuigiza na marehemu Kanumba na kuvuma zaidi katika tasnia ya filamu Bongo na sasa anajiongeza kufanya kazi nyingine katika kufikisha ujumbe katika jamii, kupitia Injili takatifu akiwa na waumini wa kutosha.
Mchungaji huyu ameanza kwa mafanikio katika kuhudumia wale wanaofika katika kanisa hilo kwa kuwafanyia maombi na kuwatoa mapepo vinyamkera na kuwaombea wenye shida mbalimbali walio tayari kwa ajili ya kumtumikia Mungu, pamoja na kuwa anatoa huduma hiyo bado ana uwezo wa kuigiza kama kawaida.
FilamuCentral