Ushoga Huu wa Aunt Ezekiel na Shamsa Ford Waibua Mambo
USHOSTI uliochipuka na kukolea hivi karibuni wa mastaa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na Aunt Ezekiel, umeibua mambo huku wengi wakihoji ulikoanzia kwa sababu haukuwahi kuwepo na kwamba hawaendani.
Wakizungumza na Ijumaa Wikienda kwa nyakati tofauti, mastaa hao walisema kuwa, wanashangazwa na watu wanaohoji urafiki wao huo ulianza lini na wengine wakisema hawapendezani ambapo Shamsa alisema kuwa, wanaoongea hivyo wamekosa vitu vya kufanya.
Kwa upande wa Aunt aliliambia gazeti hili kuwa, wanaojadili urafiki wake na Shamsa hawana jipya kwani alishakuwa na marafiki wangapi hadi waujadili huo wa sasa? “Nimeshakuwa na marafiki wengi sana. Kwa nini wajadili urafiki wangu na Shamsa?” Alihoji Aunt