Kajala Atoa Tamko Rasmi la Ndoa Yake
SUPASTAA wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ ametoa tamko rasmi kuhusu ndoa yake na mumewe, Faraji Chambo akisema kuwa hana mpango wa kurudi tena kwenye ndoa hiyo kwa kuwa hata mumewe huyo alipotoka gerezani hakuwa na muda wa kumtafuta yeye kama mkewe.
Kajala aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kama mume, ni lazima angefanya taratibu za kumuona mkewe kwani hata yeye alikuwa akienda kumuona gerezani na isitoshe anajua wazi mumewe huyo anahofia mali zake alizorudishiwa baada ya kushinda kesi. “Unajua ilibidi anitafute, lakini alikaa kimya, akaendelea na mambo yake hiyyo siwezi kurudi kwenye ndoa hiyo tena,” alisema Kajala.
Chanzo:GPL