Nisha: Sina Mpango wa Kuzaa kwa Sasa
MWIGIZAJI wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpango wa kuzaa tena kwa sababu ya kumpa malezi bora mwanaye aliyenaye.
Full Shangwe ilizungumza na Nisha ambaye alikuwa kwenye harakati za kumpeleka mtoto wake wa kike shuleni na kusema;
“Sijafikiria kuzaa mtoto mwingine kwa sasa, acha kwanza mwanangu nimpe malezi bora, kwa sasa namuandaa ili arudi shuleni kupambana,”alisema Nisha.
Chanzo:GPL