Penzi Motomoto la Dulla Makabila na Sajent Laingia Mdudu ….Wabwagana Kimya Kimya
MSANII wa filamu Bongo, Husna Iddi ‘Sajent’ ambaye alikuwa kwenye mapenzi motomoto na msanii wa singeli Dulla Makabila, uhusiano wao unadaiwa kuvunjika kutokana na kutofautiana kwenye baadhi ya mambo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao sasa si wapenzi wameshatemana ila wamekuwa wakifanya siri jambo hilo, kukwepa aibu kwa jinsi walivyokuwa wameshibana, ambapo Sajent alipotafutwa alisema kuwa yupo bize hawezi kuongelea jambo hilo.
“Hivi (anataja jina la mwandishi) hakuna wasanii wengine wenye mahusiano ambao mnaweza kuwahoji, basi naomba uwaulize hao, mimi nipo bize kwa sasa,” alisema huku Dulla alipotafutwa simu yake haikuwa hewani.