DIAMOND PLATNUMZ: Rwanda ni Nyumbani pia.
Msaani Naseeb Abdul Juma aka DIAMOND PLATNUMZ alihojiwa hivi karibuni kwenye luninga ya Rwanda (Exclusive Interview) RTV na akawamwagia sifa Kem Kem Mashabiki zake kutoka Rwanda kwa jinsi wanavyompa support katika kazi zake ya Kisanii na pia ununuzi wa bidhaa zake. Alisema ” Rwanda is my Second Home ” akiwa anamaanisha Rwanda ni Nyumbani kwake pia.
Diamond Platnumz alieleza kuwa ilikuwa ni kama mara yake tatu au nne kuwepo nchini humo. Lakini ilikuwa mara ya pili kualikwa kwenye hio exclusive interview na RTV. Diamond alielezea sababu ya kwenda Rwanda mara hii ni kwa ajili ya kutangaza bidhaa zake zikiwemo “DIAMOND KARANGA” na “CHIBU PERFUME”. Na pia Msanii huyu alitamani sana kuwa na nyumba nchini Rwanda na ikipendeza atamiliki nyumba nzuri ya kifahari kwa ajili ya mapumziko na kuishi yeye na familia yake.
Alisisitiza mziki uchukuliwe kama Ajira kubwa kwa vijana, wazazi wawaunge mkono vijana wao na utumike vizuri katika kuwasaidia wengine wenye shida na pia kutoa ajira kwa vijana.
Diamond platnumz alisema kuwa ataachia album yake itakayo itwa “BOY OF TANDALE” tarehe 23 Feburari, 2018.
Msaani diamond platnumz aliulizwa, ni jinsi gani alikuwa anamahusiano na msaani wa marekani, RISKO ROSS na alitoa wapi wazo kufanya colabo na msaani RICK ROSS hadi aliweza kutoa nyimbo kwa pamoja ambayo inaitwa “WAKA WAKA”. Diamond alisema kuwa “amebarikiwa, na kuwa anamshukuru Mungu kwa yote ,maana RICK ROSS pamoja na wasanii wengine kama vile THE MIGOS, DJ KHALID, LIL WAYNE na wengine, wana mahusiano kwa ajili ya kinywaji maarufu kilichotengenezwa ufaransa kinachoitwa BELAIRE ambacho DIAMOND PLATNUMZ ni moja wa ambassadors.
DIAMOND alisema msaani RICK ROSS alikuwa na wazo ya kufanya colabo kwajili ya kuweza kutangaza kinywaji hicho. Na waliweza kutengeneza nyimbo ambayo sasa ni maarufu sana inayoitwa “WAKA WAKA”.
Msaani DIAMOND PLATNUMZ alisema kuwa kwa mafanikio yake angependa sana kushukuru support ya familia yake , mashabiki na hasa hasa vyombo vya habari na kuwa msaani ambaye hatashukuru vyombo vya habari “ATAKUWA ANAMATATIZO YA AKILI” maana vyombo vya habari ndivyo vinao wasaidia wasanii kujulikana.
DIAMOND PLATNUMZ aliulizwa , Je angependa watoto wake pia wawe wasaani? Diamond akajibu “labda Mtoto wa kiume” akaulizwa kwanini sio wa kike ? diamond akajibu “ Mziki unastress nyingi na asingependa mwanae wakike awe na stress.
BOFYA HAPA KWA KUANGALIA INTERVIEW YA DIAMOND PLATNUMZ
CHINI:
Pia Diamond alipata nafasi ya kutembelea kituo cha watoto wenye ulemavu wa kuona na kuahidi kuwapatia msaada.