-->

Idris Awachanganya Team Wema

Hali imeanza kuwa tofauti na ya huzuni kwa mashabiki wa Wema Sepetu baada ya Idris kupost ujumbe ambao unaonesha kuwa alikuwa anategemea kupata watoto mapacha lakini haijaweza kuwa hivyo kutokana na ujauzito huo kuharibika.

IDRISS231

Zikiwa zimepita wiki kadhaa toka taarifa rasmi za watu hao kutoka kimapenzi na kuonesha walikuwa wanategemea kupata mtoto baada ya Wema Sepetu kushika ujauzito, hali imeanza kuwa tofauti na ya huzuni kwa mashabiki wa Wema Sepetu baada ya Idris kupost ujumbe ambao unaonesha kuwa alikuwa anategemea kupata watoto mapacha lakini haijaweza kuwa hivyo kutokana na ujauzito huo kuharibika.

“Ingawa mmeishi kwa siku chache wiki 13 lakini mlitokea kupendwa sana,natamani japo ningewashika ” hiki ni kisehemu kutoka katika ujumbe wa Idris Sultan aliopost kwenye Acount yake ya Intgram, ambao umeonyesha kuwa vuruga na kuwachanganya mashabiki wa Wema Sepetu ambao baadhi yao wameanza kumpa pole mrembo huku wengine wakiwa hawaamini kile alichoandika Idris na kumtaka Wema Sepetu asema jambo lolote juu ya ujauzito wake huo.

Aluminium_bussiness: Wema Sepetu pole kwa miscarriege haya fanya diet sasa urudi kuwa mrembo punguza huo uzito kabisaa, Mungu ataakujalia utapata mimba nyingine hiyo haikuwa ridhiki.

Culture_beauty: Team Wema ifike mahali tujitambue sio tupo tupo tu kama mang’ombe kwasasa inatosha.

Miyna_abdallah: Dada Wema Sepetu mimba haitangazwi kiasi hicho dadangu… Mimi mwenyewe ziliwahi kutoka mimba tatu lakini nilikuwa kila ikiingia ndugu wote watapata habari… Safari hii wameshtukia nishajifungua ila najua ni mungu amenisaidia ila macho ya watu mabaya.Nadhani umejifunza kitu sasa.

Aa042776: Wema Sepetu tuhakikishie basi nini kinaendelea, sawa mimba imetoka basi sie tunataka ukweli utujuze wewe mwenyewe.

Mbali ni hilo kupitia kipindi cha eNews kinachorushwa na EATV. Idris alisema kuwa kuna ukweli juu ya tetesi zilizokuwa mtaani kuhusiana na mpenzi wake huyo Wema Sepetu na aliwataka watanzania kuwa wavumilivu kuwa sio jambo la kukurupuka ila watatoa taarifa rasmi, na jana Idris aliweka wazi kuwa watoto mapacha aliokuwa akiwategemea kuwapata kwa bahati mbaya wamepoteza maisha, hivyo huenda ile taarifa rasmi aliyokuwa akidai ndio hii sasa.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364