-->

Wolper, Dk. Fadhili Siri Yao Yavuja

Siri imevuja! Daktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dar, Dk. Fadhili Emily amedaiwa kumponza mwigizaji Jacqueline Wolper kwa mpenzi wake wa sasa, Mkongo baada ya picha yake kukutwa kwenye simu ya mwigizaji huyo.

Wolper-Fadhil

Chanzo kilicho karibu na Wolper kimepenyeza habari kuwa Wolper ambaye yupo nchini Afrika Kusini akijivinjari na Mkongo wake, simu yake ilinaswa na Mkongo ikiwa na picha za zamani za msanii huyo akiwa na Dk. Fadhili walizopiga wakiwa mkoani Mwanza, sambamba na kuona mawasiliano yanayotia shaka kati yao.

“Huwezi amini, Wolper kamaindiwa kinoma na Mkongo. Amegundua wana mawasiliano ya siri na mbaya zaidi amekuta picha tata za Wolper na Dk. Fadhili walizopiga miaka ya nyuma ndipo Mkongo akaja juu na kumtuhumu kwamba  kama amehifadhi picha hizo, basi huenda wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu,” kilisema chanzo hicho huku kikimtumia mwandishi wetu picha hizo zilizozua ugomvi.

Baada ya kunyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Wolper bila mafanikio baada ya simu yake kuita bila kupokelewa. Alipotafutwa Dk. Fadhili, alisema yeye haoni shida kuwa na Wolper hivyo kama Mkongo amemshindwa, amuachie.

“Wolper nilimpenda na nitaendelea kumpenda. Nilishamwambia kwamba atazunguka kote lakini mume wake wa halali ni mimi,” alisema Dk. Fadhili.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364