-->

Wasanii Watoa Neno Siku ya Wanawake Duniani

IKIWA leo ndiyo maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani, wasanii wa kike wameeleza mambo mbalimbali kuhusiana na siku hiyo huku wakiwataka wanawake wenzao kuwa na msimamo katika kuendesha maisha yao.

Aunt Ezekiel  Akiwa na Mama Yake

Aunt Ezekiel Akiwa na Mama Yake

Anty Ezekiel

Mwigizaji huyo wa filamu za Bongo amewataka wanawake wenzake waache utegemezi kwa wanaume wao.

“Kuna biashara nyingi za kufanya, unaweza kuuza hata vitumbua lakini siyo kubweteka kusubiria uletewe kila kitu, kila mtu ana nafasi yake kwenye jamii, wanawake hatutakiwi kubweteka lazima tujishughulishe,” alieleza Anty Ezekiel.

Dayna Nyange

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dayna Nyange, alisema wanawake wanatakiwa kuiga njia walizotumia wanawake wenye mafanikio dunaini kote ili nao wapitie njia hizo kubadilisha maisha yao badala ya kuendelea kuogopa kila kitu.

“Mwanamke anatakiwa kutokuwa na aibu ya kutenda jema kwa maisha yake ya sasa na baadaye kwa kuiga mazuri katika elimu, siasa, biashara na yoyote yenye tija ya maendeleo,” alieleza Dayna.

Sara Mvungi

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Sara Mvungi, ameshauri wanawake waitumie siku hii kwenda hospitalini au sehemu za wazee, walemavu kwa ajili ya kuwafariji na kuwatia moyo huku akisisitiza kuanzishwa kwa umoja wa wanawake kwa ajili ya kusaidiana.

Ester Kiama

Mwigizaji wa filamu za Bongo, Ester Kiama, alisema aliwahi kufuata mkaa porini ambapo alikumbana na mazingira magumu kwa kuwa alitaka kupata kitu cha kumuwezesha kujitegemea na maisha yake na alifanikiwa.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364