Tuzo ya Lulu Yamliza Mama Kanumba
Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Filamu Afrika Mashariki, iliyotwaliwa na Mbongo,
chozi mama wa aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, tambaa na Risasi Mchanganyiko liujaze moyo wako.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mama Kanumba, muda mchache baada ya Lulu kutangazwa na waandaaji wa tuzo ambao ni African Magic Viewers Choice ‘AVCA’ kwamba yeye ni mshindi, aliwasiliana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila, ambaye naye alimtwangia simu mama Kanumba ili kumfahamisha ushindi huo ambapo mama huyo alitoa chozi.
WEWE SIKIA HII
“Sasa sijajua, yule mama alilia kwa sababu ya furaha au vipi! Maana si unajua siku za karibuni hawakuwa vizuri? Lakini inawezekana akalia kwa chuki kweli?,” kilihoji chanzo hicho.
NJIA PANDA
Pamoja na maneno yote, bado chanzo hicho kilishindwa kuweka wazi kilio cha mama Kanumba kilitokana na nini lakini kilisema kuwa, mwanamke huyo, baada ya kupokea salamu hizo, alionekana kuwaza mbali sana huku akitanabaisha kuwa, amemkumbuka mwanaye Kanumba ambapo alimtaja kama mara tatu hivi lakini pia alikumbuka ukaribu wake na Lulu.
WAMEPATANA SASA?
Chanzo kikazidi kuanika kwamba, mbali na kumjulisha mama Kanumba kuhusu ushindi wa tuzo kwa binti yake, pia aliitumia simu hiyo kumtaka mama Kanumba washirikiane kuandaa sherehe ya kumpongeza Lulu, inadaiwa mama Kanumba alikubali kwa herufi kubwa hali inayoonesha kumalizika kwa bifu.
RISASI LAWASAKA WOTE
Baada ya ubuyu huo, gazeti hili lilichacharika kuwatafuta wawili hao ili kujua nini kilijiri juu ya taarifa hiyo ya Lulu kutwaa tuzo ambayo huenda itamfunulia ukurasa mpya katika tasnia hiyo, aliyoianza kuitumia akiwa bado mdogo kiumri.
MAMA LULU HUYU HAPA
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, mama Lulu alisema alipopata taarifa za ushindi wa mtoto wake kupitia Filamu ya Mapenzi ya Mungu ‘alichizika’ kwa furaha kutokana na binti huyo kuanza kazi hiyo ya kuigiza kwa muda mrefu lakini kipindi hiki Mungu amemuona na kumshika mkono.
“Yaani nilipopata taarifa za ushindi wa mtoto wangu nilichizika kabisa kwa furaha, maana mwanangu kasota sana jamani! Mungu amemuona na mimi nazidi kumwombea, ” alisema mama Lulu.
KUHUSU KUMPIGIA SIMU MAMA KANUMBA
Kuhusu madai kwamba alimwendea hewani mama Kanumba kumhabarisha, mama Lulu alisema:
“Huwezi amini, sijazungumza na mama Kanumba kwa kipindi kirefu sana kutokana na matatizo ya hapa na pale kama binadamu, lakini niliweka bifu pembeni na kumpigia simu kumuuliza kuhusu kumpongeza mtoto wetu kwa sababu filamu hiyo aliyoshinda, naye (mama Kanumba) alishiriki kucheza, tena vizuri.”
MAMA KANUMBA SASA
Baada ya kumwacha kando mama Lulu, Risasi Mchanganyiko likamvutia ‘waya’ mama Kanumba ambapo alikiri kupigiwa simu na mwanamke mwenzake huyo japokuwa hakuwa ameelewa vizuri kuhusu tuzo hiyo. Hata hivyo, alisema anamshukuru Mungu kwa Lulu kunyakua tuzo hiyo.
“Mimi sijaelewa vizuri kuhusu tuzo yenyewe, lakini mama Lulu aliponipigia na kunipa taarifa nimefurahi na nimemshukuru Mungu kwa hilo kwa sababu ushindi huo ni wetu sote Watanzania,”alisema mama Kanumba.
KUHUSU KUTOA CHOZI
Risasi Mchanganyiko lilipoanza kumuuliza kuhusu kutoa chozi kwa taarifa hiyo, mama Kanumba aliashiria kuitoa simu yake kwenye sikio hivyo kutosikia tena na alipopigiwa tena, hakuwa akipokea.
MAWAKILI WASHINDANA SAFARI YA LULU NIGERIA
Wakati huohuo kumekuwa na mzozo wa kisheria kati ya wanasheria wawili nchini, Ado Novemba na wakili wa Lulu ambaye aliomba jina lake kupigwa ‘tintedi’, ishu ikiwa ni ile kesi inayomkabili Lulu ya kudaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia.
Ado amesema kuwa, Lulu ana zuio la kutosafiri nje ya Dar es Salaam kutoka Makahama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambako kesi itasikilizwa. Akahoji amewezaje kufika Nigeria mbali kote huko.
KAMA NI RUHUSA
Ado aliendelea kusema kuwa, mtu mwenye kesi kama ya Lulu akipewa zuio, anaweza kusafiri kwa kibali cha mahakama kama itajiridhisha.
“Lakini ili mahakama ijiridhishe inatakiwa sababu za msingi sana kama kwenda kutibiwa nje ya nchi. Kinyume cha hapo hakuna kibali,” alisema Ado.
WAKILI WA LULU
Naye wakili huyo wa Lulu alisema: “Hawezi kusafiri bila kuomba ruhusa kutoka mahakamani. Halafu mtu anaposema mpaka mahakama ijiridhishe hilo ni suala la hakimu husika. Kwani kujiridhisha ni nini?! Lulu alikwenda kufanya jambo la Watanzania wote, si lake binafsi.”
Chanzo: GPL