Prodyuza wa Going Bongo Kuchukua Wasanii Bongo
WASANII wanaochipukia wametakiwa kujitokeza katika usahili wa filamu mpya ya mshindi wa tuzo ya filamu bora Afrika Mashariki katika tuzo za Filamu za Kimataifa kwa nchi za Jahazi (ZIFF) kupitia filamu yake ya Going Bongo, Ernest Napoleon, utakaofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Usahili huo utakaoanza kwa wasanii wa kike wenye umri kati ya miaka 16 na 30 utafanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Aprili 2 majira ya jioni.
Kwa mujibu wa Ernest anayeishi Marekani kwa sasa, filamu hiyo mpya ya ‘XBaller’, itakusanya wasanii kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Watanzania na kisha watajumuishwa pamoja kwa ajili ya filamu hiyo.
Katika usahili huo wanaotaka kushiriki wanatakiwa kujiandaa kibunifu na uwezo wa kuzungumza na kuigiza mambo mbalimbali.
Mtanzania