-->

Huu Ndiyo Mchango wa Diamond kwenye lebo yake ya WCB

Msanii Diamond Platnumz amefunguka na kusema kwenye Label yake ya WCB yeye huwa anachangia vitu vidogo sana na kusema management yake chini ya Babutale na Mkubwa Fela ndiyo wanao waangalia wasanii na kuona kama wasanii hao wana vipaji na uvumilivu.

DIAMOND733

 

Akiongea na East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet bongo Diamond Platnumz amedai wakati mwingine wasanii wa label yake ya WBC wanaweza kula msoto mkali mpaka anawaonea huruma lakini huwa hawezi kuingilia kwani anatambua kuwa viongozi hao wanajua mambo mengi kwenye muziki.

“Kiukweli wasanii wanaokuja kwenye label yangu mimi huwa si mchunguzi sana, lakini management yangu ndiyo huwa inaangalia wakina boss Tale na Mkubwa Fella wao ndiyo wanaangalia huyu msanii anakipaji au hana, wao ndiyo wanajua huyu mambo iko huku au hamna. Wao wanaangalia vitu vingi wanaangalia kama msanii ni mvumilivu hivyo kuna

vitu vingi wao wanakuwa wanangalia kutokana na uzoefu wao katika muziki na kudeal na wasanii. Kuna wasanii wanaweza kula msoto mpaka unawaonea huruma lakini ndiyo hivyo ukitaka kuingilia tu watakwambiaa hapana usiingilie tuache kuna jambo tunalitizama” alisema Diamond Platnumz

Diamond Platnumz aliongeza na kusema yeye mchango wake huwa ni mdogo sana, labda katika hatua za mwisho kuona msanii yupi anastahili kutoka kwa wakati upi, au kama msanii ana mapungufu fulani yeye anaweza kuchangia mawazo labda msanii huyo afanye kitu gani ili mwisho wa siku aweze kutoka.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364