Wanawake Hatupendani Kabisa -Khadija Kopa
Msanii maarufu wa taarabu nchini Khadija Kopa amewaasa wanawake nchini kupendana na kusaidiana ili kuweza kupiga hatua za kimaendeleo.
Kopa ameyasema hayo aliposhiriki katika kipindi cha wanawake live kinachorushwa na EATV ili kuwajengea wanawake ujasiri wa kutafuta na kuepuka utegemezi hapa nchini.
”Wanawake hatupendani mimi ni mwana siasa nikiwa kwenye kura hatua za kupigiwa kura wanaume wananipa kura nyingi sana ila nikigeukia upande wa wanawake nakosa kura kabisa tena wengine wanasema huyu hana hela”
Msanii huyo ameongeza kuwa ”Wanawake tusapotiane ukiona mwezako anafanya kazi nzuri muunge mkono kuliko kurudishana nyuma na kukatishana tamaa sisi kwa sisi”.