Steve Nyerere Kutoa Movie Moja tu Mwaka Huu
Mchekeshaji na staa wa Bongo Movies, Steve Nyerere ameibuka na kusema mwaka huu atatoa filamu moja tu.
Steve Nyerere amesema anawashangaa wasanii wanaotoa movie nyingi lakini hazina ubora.
Amesema “Kuna watu wanatoa movie mpaka tatu kwa mwaka lakini zote ni mbovu”. Steve ameahidi kuwa movie hiyo atakayoitoa itakuwa ni kali sana.
Steve aliongea hayo na eNewz ya EATV