Mama Kanumba Aeleza Haya Kuhusu Lulu
Mama Steven Kanumba amesema Elizabeth Micheal ‘Lulu’ hana msaada kwake na hata sura yake ameisahau.
Akizungumza kwa uchungu katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Jumatatu hii, Mama Kanumba amesema kitu ambacho alikuwa anakihitaji kutoka kwa Lulu ni salamu pekee.
“Lulu hanisadii kitu chochote na hata sura yake nimeisahau,” alisema Mama Kanumba. “Mimi sihitaji msaada hata salamu tu inatosha,”
Pia alisema anashukuru kumuona Mama Lulu kwenye ibada ya siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba iliyofanyika Machi 7 katika makaburi ya Kinondoni.