-->

Patrick Amkumbuka Uncle Kanumba

Patrick katika pozi la picha

Patrick katika pozi la picha

Ni msanii ambaye aliibuka kupitia filamu ya This is it akiwa sambamba na mwigizaji mwenzake Jenifer huyu si mwingine ni Othuman Njaidi ‘Patrick’ vipaji vilivyoiburiwa na maremu Kanumba Patrick anasema kuwa anamkumbuka sana Kanumba kwani alikuwa mlezi kwake.

“Ni tofauti sana na Uncle Kanumba alivyotulea, yeye alitulea kama watoto wake kazini lakini watayarishaji wengine hawatupi nafasi hiyo wananichukulia kama mwigizaji tu na wala sina ndoto nyingine,” Patrick

“Kila mara ninapomkumbuka Uncle Kanumba ni tofauti kabisa na watayarishaji wengine ambao wanatuchukulia kama wasanii wengine na si watoto tunaohitaji kulelewa vema, kwa kutumia siku ya kumbukumbu ya kifo chake tunafarijika,”

Filamu ya This is It iliyomtoa Patrick katika filamu

Filamu ya This is It iliyomtoa Patrick katika filamu

Patrick anasema kuwa marehemu aliwachukulia kama familia yake huku akiwahimiza kusoma kwa bidii na kutenganisha muda wao kufanya kazi za sanaa na muda wa shule lakini wengi wanakuwa ubanaji wa muda msanii huyu yupo kidatu cha nne Kifai Mordern School Kilvya.

Kesho ni siku ya tarehe 7. April. ambayo mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ alifariki dunia, kifo kinachosadikiwa kusababishwa na msanii mwezake wa kike Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni siku muhimu kwa wasanii wote Bongo kumkumbuka gwiji huyo .

Kesho majira ya saa tisa katika makaburi ya Kinondoni familia ya Kanumba na wasanii wenzake watafanya kumbukumbu kwa ajili msanii huyo kipenzi cha wapenzi wa filamu.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364