-->

Mr.Blue: Nilipanga Kuoa Siku ya ‘Birthday’ Yangu

Staa wa bongo fleva Mr. Blue  ambaye amefunga ndoa hivi juzi na mkewe Wahyda ambapo hivi sasa wako visiwani Zanzibar kwenye fungate, ameeleza kuwa alipanga kufunga ndoa yake kwenye siku yake ya kuzaliwa.

NDOA YA MR blue-1

Mr. Blue na mkewe Wahyda

‘’Haikuwa ghafla ila ghafla kwa wananchi ila kwangu mimi ni kitu ambacho nilikuwa nimepanga karibu mwezi nyuma nilipanga nioe siku ya ‘birthday’ yangu hatukutaka nifanye kwenye ‘public’ndio maana imekuwa ghafla baada ya kuoa na kumaliza nikakaa na wakubwa wangu wakaniambia kuna watu hadi leo wanafanya uhuni na huenda wakabadilika kupitia wewe’’Alisema Blue.

kisha akasisitiza kuwa;

‘’Nilikuwa najiona mhuni kwa muda mrefu sana kuzalisha tu bila kuhalalisha nikaona ni vyema kuhalalisha’’Aliongezea Blue.

cloudsfm.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364