-->

Dayna Atoboa Sababu za Kukataa Kuolewa Mara Kadhaa

Msanii Dayna Nyange mwezi uliopita alihudhuria ndoa ya mshakaji wake Roma ilifanyika mjini Tanga, lakini pia mwezi uliopita kuna picha yake ilisambaa anaonekana ametupia shela la harusi yupo na mwanaume flani, akiizungumzia picha hiyo alisema kuwa picha ile ilipigwa kwenye maonyesho ya mavazi, je ana mtazamo gani kuhusu ishu za kufunga pingu za maisha.

dayna34

‘’Kiukweli kabisa kuna wakati natamani niwe kwenye mahusiano natamani niwe naamka na mume wangu naenda sehemu Fulani lakini najua nimemuacha mume wangu,yaani niwe mwanamke ambaye nina mume wangu,lakini kwa mazungira yaetu ya sasa hivi yanatuwia vigumu sana kuamua au kuingia kwenye mahusiano hayo kwa sababu kadhaa yawezekana viajana tumekuwa na tama nyingi au watu wamekuwa waoga wa maisha wanajikuta wamekuwa waoga kwenye mahusiano ya ndoa’’ Alisema Dyna.

‘’Kuna wanawake pia siku hizi wamekuwa wakijirahishisha sana uko na mwanaume umekutana nae mwezi mmoja unataka akuoe, unawezakukuta mwanaume anataka kukuoa lakini hujamridhia ilishawahi kunitokea kama mara tatu najikuta nakuwa muoga kwasababu nyingi ambazo nimepitia katika maisha yangu kabla kwahiyo nakuwa muoga kufanya maamuzi hayo ya kuingia kwenye ndoa kwa kutamani tu, kuna vitu vichache unatakiwa uviangalie na uvikubali kabla ya kuingia kwenye ndoa sasa unakuta havipatikani au uakuta viko nusu mwisho wa siku tunakuwa kwenye mahusiano tu ya kawaida’’ Alisema Dyna.

cloudsfm.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364