-->

Brother K Aongelea Filamu ya Kirungu Kutoka Vision One Picture

MCHEKESHAJI mahiri kutoka kundi la Futuhi Andrew Ngonyani aka Brother K amefanya tour katika vyombo vya habari kanda ya Ziwa akiinadi filamu ya Kirungu ambayo inasambazwa na kampuni mpya kabisa ya Vision One Picture kutoka Dar es Salaam, huku akitamba kuwa filamu hiyo si ya kuikosa.

Brother K mwigizaji wa Filamu akiwa katika mahojiano na mtangazaji

Brother K mwigizaji wa Filamu akiwa katika mahojiano na mtangazaji

Brother K akiongelea sinema ya Kirungu kupitia Redio Free Afrika na Kiss Fm kwa nyakati tofauti amesema kuwa filamu ya Kirungu ni kazi yenye upinzani mkubwa sana kwani anakutana na vichwa vyenye uwezo mkubwa katika uigizaji na wajuzi kweli kweli.

“Hawa Vision One Picture wamefanya jambo kubwa sana maana King Majuto alikuwa ananiogopa lakini Producer wangu Freedom akanikutanisha naye nimemkimbiza sana humo,”

“Sasa kazi yetu inaingia sokoni tarehe 9 mwezi huu siku ya jumatatu usiikose uone jinsi ambavyo nimefanya makubwa kuna Ben Blanco, King Majuto na Freedom mwenyewe,”anasema Brother K.

Sinema hiyo inasambazwa na kampuni ya kisasa kabisa ya usambazaji wa filamu Swahilihood ya Vision one Picture ya jijini Dar es Salaam na itasambazwa nchi nzima katika maduka ya filamu za Kibongo .

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364