Hii Ndiyo Kazi ya Johari Mbali na Filamu
Msanii mkongwe wa filamu, Brandina Chagula ‘Johari’ amesema nje ya filamu anafanya biashara ya mapishi ya vyakula mbalimbali lakini ni kwa oda maalum.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha filamu ya ‘RJ Company’, akiwa Vicent Kigosi, amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa, nje ya filamu yeye ni mjasiriamali wa biashara ya chakula.
“Mimi kama mimi ni mjasiriamali, kwa sasa nafanya biashara ndogo ndogo za maswala ya chakula yaani kupika. Kwa hiyo kama mtu akiwa na ofisi yake alafu anataka huduma yangu ya chakula, naandaa alafu nampelekea,” alisema Johari.
Johari amesema kazi hiyo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu na inampatia kipato kizuri kwa kuwa ni miongoni mwa kazi ambazo anazipenda pia.
Bongo5