Faiza Atoa Sababu za Kwanini Hajatoka na Mtanzania Tangu Aachane na Baba Sasha
Msanii wa filamu na Mama wa mtoto mmoja aitwae Sasha, Faiza Ally amedai hajawahi kufanya mapenzi na mtanzania yeyote toka aachane na aliyekuwa mume wake Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa madai kuwa anaogopa kuzalilishwa.
Muigizaji huyo amesema hali hiyo imekuja kutokana na matukio ya uzalilishaji wa wanawake ambayo yanaripotiwa kutokea katika sehemu mbalimbali hapa nchini.
Kupitia instagram, Faiza ameandika:
Wanaume acheni kuzalilisha wanawake, video imenisikitisha na mwanamke yoyote atakaye ipost ni mjinga, maana ana chofanya naye ni uzalilishaji. Kusema kweli toka niachane na Baba Sasha sija date na mtanzania Kwa sababu naogopa unaweza ukahisi unatongozwa kwa heri Kumbe mtu kakupania kukuzalilisha! Nimesikitishwa lkn kwa hatua zilizo chukukuliwa na serekali na juhudi za muandishi nimeshukuru sana sana! Na Niko tayari hata kuandamana kupinga wanaume wazalilishaji# na nukuu maneno kutoka bungeni #wanawake ni mama zenu#dada zenu#mabinti zenu#shangazi zenu #ACHENI KUTUZALILISHA ?