Amanda Abanwa Kuhusu Ukimwi, Afunguka
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Amanda Poshi amefungukia taarifa zinazomhusisha yeye kuugua maradhi ya Ukimwi.
Amanda amefunguka hayo baada ya kuvuja kwa picha zake zinazomuonesha akiwa amepungua mwili na kusababisha gumzo litawale kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii watu wakihusisha kukonda kwake na ugonjwa huo ndipo mwanahabari wetu alipombana, akafunguka:
“Nina desturi ya kupima kila wakati, hawanipi presha. Nimeshapima mwaka 2013 kibao na mara ya mwisho ni mwaka jana lakini hayo madai yamekuwa yakiibuka mara kwa mara wananiboa kweli mbaya zaidi hao wanaolazimisha nipime wao wenyewe hawapimi.
“Nilipokuwa mnene presha ilikuwa inashuka kila mara, namshukuru Mungu kwa sasa nimeanza gym niko imara, nimepungua mwili vizuri.”
baada ya kusema hayo Amanda alimtumia mwanahabari wetu vyeti vyake mbalimbali vyenye majibu ya Ukimwi vikionesha yupo safi.
Chanzo:GPL