Lulu Kusaka Tuzo Oscar na Filamu ya ‘Ni Noma’!
ILE Filamu kubwa ya Ni Noma ‘Huyu Demu ni Feki’ kutoka kwa mwanadada Nyota katika tasnia ya filamu Swahilihood Elizabeth Michael ‘Lulu’ ipo tayari kuingia sokoni baada ya kutengenezwa katika viwango vya kimataifa, kazi hiyo inakwenda kusaka tuzo kubwa kabisa ya Oscar.
Filamu ya Ni Noma chini ya utayarishaji wa mtayarishaji mahiri kabisa katika utayarishaji wa filamu za kimataifa kutoka Swahilihood Staford Kihore kuanzia tarehe 15. July 2016 itaingia sokoni rasmi ikiuzwa katika teknolojia mpya ya Proinbox.
“Sinema ya Ni Noma ni kazi nzuri sana na naamini kuwa ina sifa za kuingia katika tuzo za Oscar na kuibuka na ushindi katika category mbalimbali ni kazi ambayo inastahili kuniongezea tuzo,”anasema Lulu.
Msanii huyo mwaka huu aliweza kuibuka kidedea katika tuzo za AMCA 2016 huko Lagos Nigeria kupitia filamu yake ya mapenzi ya Mungu na sasa anakuja na filamu ya Ni Noma kuelekea tuzo za Oscar atatisha sana.
Sinema ya Ni Noma ‘Demu huyu ni Feki’ imewashirikisha vijana kama Isalito, Baba James, Kulwa Kikumba ‘Dude’, nyota kutoka mradi mkubwa kabisa wa kukuza vipaji wa Tanzania Movie Talent (TMT) ambapo wameonyesha uwezo mkubwa sana katika sinema hiyo.
FC