Mimi na Shamsa Ford Tuliachana Vizuri – Nay wa Mitego
Nay wa Mitego amezungumzia jinsi alivyoachana na aliyekuwa mpenzi wake Samsha Ford baada ya mwanadada huyo kudai hataki tena kutoka kimapenzi na mastaa.
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, rapa huyo alisema licha ya kuachana na mwanadada huyo bado ni mshkaji wake na wanapiga stori kama kawaida.
“Mimi binafsi sijui alikuwa anamaanisha nini lakini kitu ambacho naweza kusema mimi na Shamsa bado ni washkaji na hatuwezi kuja kuwa maadui hata siku moja licha ya kuachana,” alisema. “Hatuna ugomvi lakini pia sijui alikuwa na mahusiano na staa gani before? Labda ndiyo maana anaongea hivyo ila mimi tuliachana vizuri.”
Aliongeza, “Kuhusu mimi sijamtenda hata yeye hajanitenda ndiyo maana mpaka leo tunaendelea kuongea japo kuwa labda yeye ana kitu anacho moyoni hicho siwezi kujua ila mimi ninachojua nazungumza naye poa tu.”
Kabla ya kuachana wawili hao walichukua muda mrefu kuweka wazi mahusiano yao.
Bongo5