Wema Sepetu Amuombea Kura Diamond kwenye Tuzo za BET
Mbali na tofauti zao na Team zao mtandano, staa wa bongo miovie, Wema Sepetu amewaomba mashabiki wake wampigie kura mpenzi wake wa zamani, Diamond Platnumz ambaye anawania tuzo za BET kwenye kipengere cha Best International Act: Africa.
Wema aliandika haya kwenye ukurasa wakewa Instagram;
“Uzalendo ndo unaotakiwa… Tanzania Kwanza Vingine Baadae… Ama nene…? Vote Vote Vote….,” ameandika Wema kwenye picha ya BET Awards
Mashabiki wengi amempongeza wema kwa uzalendo aliouonesha.
Katika kipengele hicho Diamond atachuana na wakali wengine kutoka Afrika kama Wizkid, Yemi Alade wa Nigeria, AKA, Cassper Nyovest na Black Koffie wa Afrika Kusini na wengine wawili.